Pages

ELIMU KWANZA.

ELIMU KWANZA.
FEDHA SIO KIPAUMBELE CHETU.

Monday 10 March 2014

BABU YANGA SC ASEMA AL AHLY HII SI LOLOTE NA HADHANI KAMA ITAVUKA HATUA IFUATAYO

Na Tarek Talaat, Alexndria
KOCHA Mkuu wa klabu ya Yanga SC ya Tanzania, Mhoalnzi Hans Van der Pluijm amesema kwamba vigogo wa Misri Al Ahly wamepoteza makali yao na si timu tisho tena ile aliyokuwa anaijua yeye, licha ya kuitoa timu yake jana kwa penalti mjini Alexandria.
“Ilivyo, Al Ahly hii si timu kali tena ambayo sote tulikuwa tunaijua na ikiwa wataendelea kucheza kama hivi katika hatua ijayo, nina uhakika watataabika,”.
“Tulikuwa karibu kuwatoa nje ya mashindano, lakini penalti ni mchezo wa bahati, na ninajivunia kiwango chetu,”alisema Pluijm baada ya mechi jana.

Hawana kitu; Hans van der Pluijm kulia akiwa na Msaidizi wake, Charles Boniface Mkwawsa kushoto jana Uwanja wa Border Guard. Mholanzi huyo amesema AL Ahly ya sasa haina makali

Pamoja na hayo, kocha wa Al Ahly, Mohamed Yousef amesema inabidi awashukuru wachezaji wake baada ya mechi, lakini amewataka kuacha kufikiria hatua ijayo ya Ligi ya Mabingwa Afrika na badala yake kuekeleza nguvu zao kwenye Ligi ya Misri.
Baada ya kuitoa Yanga SC, timu hiyo yenye maskani yake mjini Cairo itakutana na Al Ahly Benghazi kuwania kuingia Hatua ya makundi ya michuano hiyo.

Alikosa na akachomesha; Mbuyu Twite akimsindikiza Sayed Moawad kwenda kuifungia Al Ahly. Twite baadaye alikosa penalti ya mwisho ya Yanga na mchezo ukaisha


Walikosa; Oscar Joshua kushoto na Said Bahanuzi kulia wanaoangalia kamera walikosa penalti jana

Ahly ilishinda 1-0 jana baada ya dakika 90 Uwanja wa Border Guard (Haras Hodoud) na kufanya sare ya jumla ya 1-1 kutokana na Yanga pia kushinda 1-0 katika mchezo wa kwanza Dar es Salaam na katika mikwaju ya penalti wakashinda 4-3.
Yanga SC tayari ipo Cairo ikisubiri usafiri wa kurejea Dar es Salaam kuelekeza nguvu zao kwenye Ligi Kuu ya Vodacom Tanzania Bara, ambako wanakabiliwa na ushindani mkali kutoka kwa Azam FC katika mbio za ubingwa.

No comments:

Post a Comment