Pages

ELIMU KWANZA.

ELIMU KWANZA.
FEDHA SIO KIPAUMBELE CHETU.

Saturday 15 March 2014

DANIEL STURRIDGE MCHEZAJI BORA WA MWEZI ENGLAND, SAM ALLARDYCE KOCHA BORA

MSHAMBULIAJI wa Liverpool, Daniel Sturridge ameshinda tuzo ya Mchezaji Bora wa Ligi Kuu ya England kwa mwezi Februari, baada ya kufunga mabao matano katika mechi nne.
Nyota huyo ameisaidia Liverpool kushinda dhidi ya Swansea na Fulham pamoja na kuitandika mabao 5-1 Arsenal timu hiyo ya Anfield ikiweka hai matumaini ya kutwaa ubingwa.
Kocha wa West Ham, Sam Allardyce, ameshinda tuzo ya Kocha Bora wa Mwezi baada ya kuiongoza timu yake kushinda mechi nne.

Mkali wa mwezi: Daniel Sturridge akiwa na tuzo ya Mchezaji Bora wa Februari
Mshindi: Sam Allardyce ameiongoza West Ham kuingia kwenye 10 Bora kwa kushinda mechi nne mwezi uliopita
VINARA WA FEBRUARI LIGI KUU ENGLAND
Daniel Sturridge
Feb 2 - West Brom 1-1 Liverpool (alifunga bao moja)
Feb 8 - Liverpool 5-1 Arsenal (alifunga bao moja)
Feb 12 - Fulham 2 - 3 Liverpool (alifunga bao moja)
Feb 23 - Liverpool 4 - 3 Swansea (alifunga mabao mawili)
West Ham
Feb 1 - West Ham 2-0 Swansea
Feb 8 - Aston Villa 0-2 West Ham
Feb 11 - West Ham 2-0 Fulham
Feb 22 - West Ham 3-1 Southampton

No comments:

Post a Comment