Rooney alikosa mechi ya Ligi Kuu England United ikiifunga mabao 4-0 Newcastle mwishoni mwa wiki kutokana na maumivu ya mguu, lakini sasa kuna uwezekano kesho akacheza
Ryan Giggs pia alifanya mazoezi baada ya kukosa mechi dhidi ya Newcastle, lakini Marouane Fellaini, ambaye alitolewa nje Uwanja wa St James Park baada ya kuumia na Rafael hawakushiriki mazoezi leo.
Baada ya sare ya 1-1 nyumbani, United sasa wanatakiwa kushinda ugenini dhidi ya Bayern ili kutinga Nusu Fainali.

Mazoezi makali: Rooney akifanya mazoezi kuelekea mchezo wa marudiano na Bayern Munich

+12
Rooney alishiriki mazoezi kikamilifu

Rooney ameonekana kusahau kabisa kuhusu maumivu

Rooney ameonekana yuko fiti kwa ajili ya mchezo huo

Kocha wa Manchester United, David Moyes ameonekana kufurahia kurejea kwa Rooney
No comments:
Post a Comment