Pages

ELIMU KWANZA.

ELIMU KWANZA.
FEDHA SIO KIPAUMBELE CHETU.

Thursday, 3 October 2013

Rafael Nadal akaribia kushika nafasi ya kwanza kwa Ubora wa Tennis Duniani upande wa Wanaume


Mchezaji Tennis nambari mbili kwa ubora Duniani Rafael Nadal


Mchezaji wa Tennis ambaye ni raia wa Hispania Rafael Nadal huenda akareja kwenye nafasi yakwanza katika orodha ya Wachezaji Bora Wanaume wa mcheo huo baada ya kufanikiwa kutinga hatua ya Robo Fainali ya mashindano ya China Open.
Nadal anayeorodheshwa katika nafasi ya pili kwa ubora wa Tennis upande wa wanaume ametinga kwenye Robo Fainali ya China Open kufuatia kumchakaza bila huruma Philipp Kohlschreiber baada ya kumfunga kwa seti mbili kwa bila.

Kohlschreiber alikumbana na kichapo kwa kufungwa seti ya kwanza kwa sita nne lakini seti ya pili alionekana kupambana na kutoa upinzani kwa Nadal lakini mwisho akafungwa kwa saba sita.

Nadal anatarajiwa kumuondoa Novak Djokovic kwenye nafasi ya kwanza ya ubora wa Tennis upande wa wanaume iwapo tu atafanikiwa kutinga hatua ya fainali ya mashindano ya China Open.

Bingwa huyo wa US Open anatarajiwa kuwa na kibarua kwenye hatua ya Robo Fainali pale atakapokumbana na mchezaji kutoka nchini Italia Fabio Fognini ambaye hadi kutinga hatua hiyo ameonesha kiwango kizuri.

Nadal amekuwa na rekodi nzuri kwenye michezo yake akishinda michezo ishirini na nne aliyocheza kwenye viwanja mbalimbali kwa mwaka 2013 kitu kinachochangia kumfanya arejee kwenye nafasi ya kwanza.

Tangu Nadal arejee uwanjani baada ya kukabiliwa na maumivu mnamo mwezi Februari ameweza kushinda mataji kumi tofauti kati ya mataji kumi na mbili aliyoshiriki kwa muda huu aliorejea.

Nadal anaomba Djokovic asishinde taji lolote halafu yeye aweze kutinga fainali ya michuano ya China Open ili aweze kupata kushika nafasi ya kwanza kwenue ubora wa Tennis upande wa wanaume.www.tabasamuleo.blogspot.com

No comments:

Post a Comment