Pages

ELIMU KWANZA.

ELIMU KWANZA.
FEDHA SIO KIPAUMBELE CHETU.

Thursday 3 October 2013

DAKTARI WA SIMBA ATHIBITISHA KUPONA KWA HENRY NA CHOLO



Henry Joseph

DAKTARI wa Simba, Yassin Gembe amemkabidhi Kocha wa Simba, Abdallah Kibadeni wachezaji wawili kiungo, Henry Joseph na nahodha Nassor Said ‘Cholo’.
Henry mchezaji tegemeo wa kikosi hicho alishindwa kucheza mechi mbili zilizopita kutokana na kusumbuliwa na majeruhi ya mguu pamoja na mkongwe mwenzake, Nassor Said ‘Cholo’ naye amepona ingawa hali ya Issa Rashid ‘Baba Ubaya’ ndiyo bado haijatengemaa.
Henry alisema: “Namshukuru Mungu nimeanza mazoezi na hali yangu ni nzuri kiafya. “Ninachosema sina wasiwasi na nawaambia mashabiki watulize presha, nimepona tayari kwa lolote,”alisema Henry na kuongeza hata mechi yao ya keshokutwa Jumamosi na Ruvu Shooting akipewa nafasi na kocha atacheza.
Naye Cholo alisema: “Kama unavyoniona nafanya mazoezi, nimepona sina tatizo lolote tena, majeruhi yaliyokuwa yananisumbua yamepona.”
Daktari wa Simba, Yassin Gembe alisema: “Henry na Cholo wamepona, suala la kucheza au kutocheza hilo ni la kocha.”www.tabasamuleo.blogspot.com

No comments:

Post a Comment