Kocha Mkuu wa Manchester United David Moyes akifanya mkutano wa waandishi wa habari
Kocha Mkuu wa Klabu ya Manchester United David Moyes amejitetea na kusema kwa sasa anaendelea kusaka Kikosi cha kwanza kauli aliyoitoa baada ya kukosolewa vikali na Kocha wa Shakhtar Donetsk Mircea Lucescu aliyesema hakuna sababu ya kubadili wachezaji kila siku. Moyes ambaye amekuwa akipata matokeo mabovu kwenye michezo ya Ligi Kuu nchini Uingereza amejikuta akikosolewa vikali kutokana na tabia yake ya kubadili wachezaji wa kikosi cha kwanza kitu ambacho kinatajwa kuwa chanzo cha matokeo mabaya.
Kocha huyo wa Manchester United Moyes ametetea hatua yake ya kufanya mabadiliko ya kika kukicha kwenye kikosi chake akisema anajitahidi kuchanganya wachezaji wazoefuna wale vijana ili kuwa na kikosi imara zaidi.
Moyes amesema mpango wake utaendelea kwani ana imani kabisa mkakati huo utamsaidia hapo baadaye atakapokuwa na wachezaji wote wenye uzoefu na watakuwa na uwezo wa kucheza katika michezo mbalimbali.
Manchester United imeshafungwa michezo mitatu kati ya sita ya Ligi Kuu Nchini Uingereza kitu ambacho kimemfanya akabiliane na ukosoaji na wengine kuhofia huenda klabu hiyo ikawa na wakati mgumu msimu huu.
Moyes atakuwa na kibarua cha kuiongoza Manchester United kwenye mchezo wa pili wa Ligi ya Mabingwa Barani Ulaya mbele ya Shakhtar Donetsk huku akiwa na kumbukumbu ya kushinda mchezo wa kwanza mbele ya Bayer Leverkusen.
Utetezi wa Moyes imekuja baada ya Kocha wa Shakhtar Donetsk Lusecu kusema Manchester United imeingia kwenye matatizo ya kupata matokeo mabaya kutokana na mabadiliko ya wachezaji yanayofanywa mara kwa mara.
Moyes ameendelea kujitetea kwa kusema hata Kocha aliyemtangulia Sir Alex Ferguson alikuwa anafanya mabadiliko ya wachezaji wake lakini hakuna matatizo yoyote yaliyotokea hivyo naye ataendelea na mpango wake.www.tabasamuleo.blogspot.com
No comments:
Post a Comment