Pages

ELIMU KWANZA.

ELIMU KWANZA.
FEDHA SIO KIPAUMBELE CHETU.

Tuesday 11 February 2014

REAL YATINGA FAINALI KOMBE LA MFALME KWA MABAO YA RONALDO

REAL Madrid imefanikiwa kuingia Fainali ya Kombe la Mfalme baada ya usiku wa jana kuizamisha Atletico Madrid kwa mabao 2-0 katika nusu Fainali ya pili.
Shukrani kwake Mwanasoka Bora wa Dunia, Cristiano Ronaldo aliyefunga kwa penalti mara mbili dakika ya saba na 16 na kufanya vigogo hao wa Hispania wasonge mbele kwa ushindi wa jumla wa mabao 5-0.
Real sasa inaweza kukutana na barcelona katika fainali ya michuano hiyo Aprili 19 mwaka huu.

We mkali: Sergio Ramos (kulia) akifurahia na Cristiano Ronaldo baada ya kufunga jana
Lakini alitoka: Ronaldo alitoka uwanjani dakika ya 75 kumpisha kinda mwenye kipaji Jese

No comments:

Post a Comment