Pages

ELIMU KWANZA.

ELIMU KWANZA.
FEDHA SIO KIPAUMBELE CHETU.

Friday 24 January 2014

MOYES ANAVYOHAHA DUNIA NZIMA KUIIMARISHA MAN UNITED...JANA ALIKUWA KWENYE MECHI YA BAYERN KUANGALIA WACHEZAJI

UNITED...JANA ALIKUWA KWENYE MECHI YA BAYERN KUANGALIA WACHEZAJI
KOCHA David Moyes alisindikizwa Uwanja wa Borussia Monchengladbach na wakala wa Toni Kroos jana usiku na inaaminika ilikuwa katika harakati za usajili.
Mshambuliaji wa Bayern Munich, Mario Mandzukic na kiungo wa Moenchengladbach, Patrick Herrmann inaaminika ndio wachezaji ambao kocha huyo wa Manchester United alikuwa anawafuatilia akiwa ameketi jukwaani Borussia Park kuangalia mchezo wa Bundesliga ambao wageni walishinda 2-0.
Lakini pamoja na hayo imevuma sana kwamba Kroos ndiye chaguo la kwanza la Moyes baada ya kuonekanana wakala wake, Sascha Breese kwenye mechi hiyo.

Mchapa kazi: Kocha wa Manchester United, David Moyes akiwa na wakala wa Toni Kroos kulia nchini Ujerumani

Anajiridhisha? David Moyes (kushoto) akitaniana na kocha wa zamani wa Bayern, Jupp Heynckes (katikati)


Mjadala mzito? David Moyes anafahamu anamuhitaji nani kuimarisha kikosi chake kabla ya mwishoni mwa January

+10
Anakuja? Mshambuliaji wa Monchengladbach, Max Kruse (kushoto) anatakiwa na United


Wafungaji: Thomas Muller (kulia) na Mario Gotze (wa pili kushoto) walikuwa mashujaa wa Bayern kwa mara nyingine

Mkali; Max Kruse (katikati) anaweza kuongeza makali safu ya ushambuliaji ya United

Anavutia; Patrick Herrmann aligongesha mwamba timu yake ikifungwa na Bayern Munich

Anaweza kuondoka: Mario Mandzukic (kushoto) anaweza kuruhusiwa kuondoka baada ya Bayern Munich kumsajili Robert Lewandowski


Mwenye mpira: Javi Martinez (kushoto) anaweza kuimarisha ngome ya United katika safu ya kiungo

No comments:

Post a Comment