Kocha wa mpira Kennedy Mwaisabula leo ametangazwa rasmi kuwa kocha wa timu ya Villa Squard ya Magomeni,timu hiyo inashiriki ligi daraja la kwanza.
''Ni kweli nimechaguliwa kuwa kocha wa Villa Squard hadi mwishoni mwa raundi yapili ya ligi daraja la kwanza, malengo yangu makubwa mara tu baada ya kupewa nafasi hii ni kuhakikisha timu hii kongwe inapanda ligi kuu mwakani''.
Hii leo Mwaisabula ameiongoza Villa kuifunga Ashanti mabao 2-1 kwenye mchezo wa kirafiki uliopigwa kwenye uwanja wa karume jijini Dar Es Salaam.
Je wajua ?
Kenny Mwaisabula amezifundisha karibia timu zote za Dar Es Salaam isipokuwa Simba.
Mwaisabula alijiunga na timu ya Cargo mwaka 1997 na kudumu nayo hadi mwaka 1999 na kufanikiwa kuipandisha kutoka ligi daraja la tatu hadi ligi daraja la kwanza,timu hiyo ya Cargo ilikuwa na wakali kama Nathaniel Elia,Jeseph Simon 'Dibro',Jaafar Abbas,Hussein Mataka na Godfrey Magori.
Mnamo mwaka 2000 alijiunga na timu ya IPP na kuiwezesha kuchukua ubingwa wa ligi daraja la tatu ngazi ya mkoa ikiwa na kikosi cha kina Juma Kaseja,Nico Nyagawa,Ally Mkongwe na Tito Andrew.
Mwaka 2000-2001 aliifundisha Ashanti ilipokuwa ligi daraja la tatu,baada ya hapo akahamia Bandari ya Mtwara na kufanikiwa kuingia ligi ya nane bora akiwa kikosi cha kina Semmy Kessy,Shabani Kisiga,Shekuwe Kibwana,Hassani Banyai na Simon Bute
Mwaka 2002-2003 alikuwa na Kikosi cha Vijana ya Ilala cha kina Ally mpemba,issa manofu,thomas kipese na Habib Kondo.
Mwaka 2004-2005 alikinoa kikosi cha Yanga kabla ya mwaka 2005 hadi 2006 kukinoa kikosi cha Twiga Stars kabla ya kurejea kikosi cha Ashanti Utd mwaka 2007 akiwasajili kina Ramadhani Chombo'Redondo',Abdulrahim Humud,Juma Nyoso,Godfrey Taita,Shabani Chogo na Patrick Mrope.
Mwaisabula anarejea Villa Squard kwa mara ya pili baada ya kuifundisha mwaka 2010 kwenye ligi kuu ya Vodacom ambapo alipewa jukumu la kuibakisha ligi kuu lakini ikshindikana.
No comments:
Post a Comment