Pages

ELIMU KWANZA.

ELIMU KWANZA.
FEDHA SIO KIPAUMBELE CHETU.

Saturday 30 November 2013

Poulsen: Uwanja ulituangusha


Nairobi. Kocha wa Kilimanjaro Stars, Kim Poulsen amesema mipira ya juu pamoja na Uwanja wa Kenyatta uliopo Machakos kujaa maji ndiyo kilichoifanya timu yake kushindwa kuisulubu Zambia.


Stars ilitoa sare ya bao 1-1 na Zambia kwenye mechi yake ya kwanza ya kundi B ambayo ilitoa nafasi kwa Burundi iliyoichapa Somalia mabao 2-0 kuongoza kundi.


Poulsen alisema,”Kipindi cha kwanza tulikuwa tunapiga mipira mirefu ile siyo staili yetu, ndiyo maana timu ilishindwa kucheza mpira mzuri.”

“Hata sura nyingi mpya kwenye kikosi cha kwanza zilifanya staili ya mchezo kubadilika na hali ya uwanja pia, lakini ikabidi kipindi cha pili tuingie na mikakati mipya ambayo ilisaidia tukatuliza mpira chini na mambo yakaonekana, ingawa bado tulikosa nafasi nyingi za kufunga,”alisema.


Kocha huyo hakulaumu mchezaji yeyote, lakini aliahidi kufanya mabadiliko kadhaa kwenye kikosi kitakachocheza na Somalia Jumapili kwa vile ushindi ni lazima.


“Lazima tufanye mabadiliko kutokana na staili ya mchezo na ushindi unatakiwa,”alisisitiza Poulsen huku akimsifu kipa wake, Ivo Mapunda kwa kucheza mipira ya juu.


Stars walilazimika kucheza mipira ya juu katika kipindi cha kwanza cha mechi ya Zambia kutokana na maji yaliyokuwa yamejaa uwanjani ambayo yalikuwa yakipunguza kasi ya mchezo na kusababisha wachezaji kutumia nguvu nyingi hususani viungo.

Stars ina pointi moja kwenye kundi lake sawa na Zambia yenye straika Felix Katongo.

No comments:

Post a Comment