Pages

ELIMU KWANZA.

ELIMU KWANZA.
FEDHA SIO KIPAUMBELE CHETU.

Wednesday 27 November 2013

MAN UNITED YAFANYA MAUAJI, YAWAPIGA WAJERUMANI 5-0 NYUMBANI KWAO









wachezaji wa Manu wakishangilia moja ya magoli yao
Wyne Rooney na Giggs wakifurahia ushindi

Kagawa akikata mbuga kuelekea kutafuta goli

MANCHESTER United imefanya mauaji makubwa ugenini, baada ya kuitandika Bayer Leverkursen mabao 5-0 nchini Ujerumani katika mchezo wa Ligi ya Mabingwa ya Ulaya.

Mabao ya United usiku huu yamefungwa na Valencia dakika ya 22, Spahic aliyejifunga dakika ya 30, Evans dakika ya 65, Smalling dakika ya 77 na Nani dakika 88.

Wayne Rooney ndiye alikuwa nyota wa mchezo kutoka na kupika mabao manne katika ushindi huo ambao haukutarajiwa.

Kikosi cha Manchester United kilikuwa: De Gea, Smalling, Ferdinand, Evans, Evra/Buttner dk70, Jones, Giggs, Valencia/Young dk80, Kagawa, Nani na Rooney/Anderson dk80.

Bayer Leverkusen: Leno, Donati, Spahic, Omer Toprak, Can, Bender/Kohr dk81, Reinartz/Hegeler dk70, Rolfes, Castro, Son Heung-min/Derdiyok dk70 na Kiessling

No comments:

Post a Comment