Pages

ELIMU KWANZA.

ELIMU KWANZA.
FEDHA SIO KIPAUMBELE CHETU.

Friday 20 September 2013

"Yanga yaapa ushindi dhidi ya Prisons"





By MWANDISHI WETU

Wachezaji wa Yanga walikiri kwamba hawakuwahi kukumbana na presha kubwa ya mashabiki wa timu pinzani mkoani kama ilivyokuwa wikiendi iliyopita jambo ambalo linawafanya wajiulize mara mbili kabla ya kurudi uwanjani ingawa wadau wa Mbeya wanadai kwamba Prisons haina mashabiki wengi kama Mbeya City.
WACHEZAJI wa Yanga wakiongozwa na nahodha wao, Nadir Haroub ‘Cannavaro’ wametangaza hali ya hatari kwa Prisons kwamba iwe isiwe hata kama vurugu zitajirudia, lazima washinde.

Lakini vuta pumzi kwanza. Kabla ya kushuhudia mechi za Ligi ya Mabingwa Ulaya, kesho Jumatano usiku, tayari utakuwa umejua vitu vitano muhimu vya kuvutia kwenye Ligi Kuu Bara msimu huu, zitachezwa mechi saba siku hiyo hiyo.


Kwanza; Yanga ipo Mbeya ikicheza na Prisons kwenye Uwanja wa Sokoine, inarudi kwenye uwanja huo ambao ilikumbana na presha kubwa ya mashabiki wa Mbeya City Jumamosi iliyopita na kuambulia sare ya bao 1-1.



Wachezaji wa Yanga walikiri kwamba hawakuwahi kukumbana na presha kubwa ya mashabiki wa timu pinzani mkoani kama ilivyokuwa wikiendi iliyopita jambo ambalo linawafanya wajiulize mara mbili kabla ya kurudi uwanjani ingawa wadau wa Mbeya wanadai kwamba Prisons haina mashabiki wengi kama Mbeya City.


Nahodha wa Yanga, Nadir Cannavaro alisema: “Makonde nje ya uwanja watupige tu, lakini kwa hizi pointi tatu, lazima kitaeleweka.”


Wachezaji wa Yanga wameapa kuwa kilichowatokea Jumamosi dhidi ya Mbeya City hawatakubali kiwatokee tena dhidi ya Prisons.


Pili; Mgambo haijawahi kufunga bao hata la kuotea kwenye Uwanja wa Taifa jijini Dar es Salaam. Itakuwa kwenye uwanja huo ikicheza na Simba, imecheza mechi mbili tu kwenye uwanja huo msimu uliopita na ikapoteza zote dhidi ya Yanga na Simba.


Simba itakuwa na viungo mahiri wanaojua kuuchezea mpira kama Henry Joseph, Jones Mkude na Amri Kiemba sawa na mastraika mwenye uchu, Betram Mwombeki na Mrundi Amis Tambwe.


Tatu;Timu maarufu zaidi kwa sasa na yenye mashabiki wengi ya Mbeya City inacheza mechi yake ya kwanza ugenini tangu ligi ianze. Itaenda Manungu, Morogoro kwa Mtibwa Sugar yenye straika mkongwe, Mussa Mgosi.


Mbeya City ilitoka suluhu na Kagera Sugar, ikaichapa Ruvu Shooting mabao 2-1 kabla ya kutoka sare ya bao 1-1 na Yanga.


Nne; Pwani kuna mechi ya watani wa jadi. JKT Ruvu ambayo haijapoteza mchezo hata mmoja tangu ligi ianze na ndiyo inayoshika usukani katika msimamo wa ligi, itacheza na mtani wake Ruvu Shooting kwenye Uwanja wa Mabatini, Mlandizi.


Tano; Ashanti United ambayo ‘inachukia’ kushinda mechi imejikita mkiani kwenye msimamo wa ligi na itacheza na timu ngumu ya Azam ambayo itakuwa inacheza kwa mara ya kwanza kwenye uwanja wake wa Chamanzi baada ya kuanzia Morogoro, Tabora na Kagera.
JKT Oljoro ambayo ilipewa ofa ya kucheza mechi tatu za kwanza kwenye uwanja wake mjini Arusha na kuchemsha zote dhidi Coastal Union, Simba na Rhino Rangers italazimika kuondoka Arusha bila kupenda.  Itaanzia Kagera kesho Jumatano, irudi Dar es Salaam halafu ipenye iingie Tanga. Watu wa Arusha wataiona mwezi ujao.
Rhino Rangers ambayo haijawahi kushinda mechi ya ligi ugenini, itakuwa Tanga kwa mara ya kwanza ikicheza kwenye Uwanja wa Mkwakwani ambako italazimika pia kusubiri hapohapo wikiendi ijayo kucheza na Mgambo.

No comments:

Post a Comment