Pages

ELIMU KWANZA.

ELIMU KWANZA.
FEDHA SIO KIPAUMBELE CHETU.

Friday 20 September 2013

Mwombeki: Nikichezeshwa na Henry Joseph ni balaa




STRAIKA wa Simba, Betram Mwombeki ametamka kwamba kiungo Henry Joseph Shindika ni bonge la mchezaji na tangu aanze kuichezea Simba iwe kwenye ligi au mazoezi amegundua vitu vingi kwake.


“Kuna viungo wengi Simba, nawakubali uwezo wao kila mmoja na mchango kwenye timu, lakini kilichonivutia zaidi ni uwezo wa Henry anapokuwa uwanjani, ana nguvu, akili, uzoefu na ameuzoea mpira. Anajua ni wapi akuwekee mpira kutokana na kasi na mbinu ulizonazo mshambuliaji,” alisema Mwombeki.


“Naamini tukizidi kuwa naye karibu tutajifunza mengi na pia tutapata mabao mengi pamoja na ubingwa wa ligi msimu huu kirahisi zaidi, anajua wapi pa kumuwekea straika mpira afunge,” alisema Mwombeki mwenye malengo ya kufunga jumla ya mabao 27 msimu huu wa ligi.


Mwombeki alifunga bao la pili kwenye mechi ya ligi Jumamosi iliyopita dhidi ya Mtibwa huku la kwanza likifungwa na Henry Joseph.

No comments:

Post a Comment