UNITED...JANA ALIKUWA KWENYE MECHI YA BAYERN KUANGALIA WACHEZAJI
KOCHA David Moyes alisindikizwa Uwanja wa Borussia Monchengladbach na wakala wa Toni Kroos jana usiku na inaaminika ilikuwa katika harakati za usajili.
Mshambuliaji wa Bayern Munich, Mario Mandzukic na kiungo wa Moenchengladbach, Patrick Herrmann inaaminika ndio wachezaji ambao kocha huyo wa Manchester United alikuwa anawafuatilia akiwa ameketi jukwaani Borussia Park kuangalia mchezo wa Bundesliga ambao wageni walishinda 2-0.
Lakini pamoja na hayo imevuma sana kwamba Kroos ndiye chaguo la kwanza la Moyes baada ya kuonekanana wakala wake, Sascha Breese kwenye mechi hiyo.

Mchapa kazi: Kocha wa Manchester United, David Moyes akiwa na wakala wa Toni Kroos kulia nchini Ujerumani