Thursday, 23 January 2014
KUUMIA KWA FALCAO NI PIGO KWA COLOMBIA & KOMBE LA DUNIA.

Habari mbaya leo kwenye michezo ni kuhusu majeraha ya mshambuliaji Radamel Falcao aliyoyapata jana usiku kwenye mchezo kati ya timu yake ya Monaco dhidi ya timu ya ligi daraja la nne ya Chasselay kwenye kombe la Ufaransa.
Wednesday, 22 January 2014
MESSI AWA BONGE LA MPISHI BARCA IKIITANDIKA 4-1 LEVANTE ILIYOTOKA NAYO SARE JUMAPILI
TIMU ya Barcelona imemaliza hasira zake za sare ya Jumapili na Levante kwa kuifumua timu hiyo mabao 4-1 usiku huu kwenye Robo Fainali ya kwanza ya Kombe la Mfalme Uwanja wa Ciutat de Valencia.
Mkali wa mabao wa Barca, Lionel Messi amecheza mechi ya 400 katika timu hiyo Katalunya usiku huu, ambazo ndani yake ameshinda mataji sita ya La Liga na matatu ya Ligi ya Mabingwa.
Messi alifanya kazi nzuri akitoa mchango kwa mabao yote manne, ikiwemo hat-trick ya Cristian Tello. Wenyeji walitangulia kupata bao lililofungwa na mchezaji wa zamani wa Liverpool, Nabil El Zhar.
Juanfran alijibabatiza mpira uliopigwa na Messi na akaudondoshea kwenye nyavu zake mwenyewe kuisawazishia Barca- kabla ya Tello kufunga mara tatu mfululizo kuipa ushindi mtamu timu yake.

Mpishi: Lionel Messi (kulia) akishangilia baada ya kumsetia Cristian Tello (katikati) kufunga hat trick katika ushindi wa Barcelona wa 4-1 dhidi ya Levante

KENNY MWAISABULA: 2010 NILIPEWA JUKUMU LA KUIBAKISHA LIGI KUU VILLA SQUARD IKASHINDIKANA,SASA NIMEPEWA JUKUMU KUIPANDISHA LIGI KUU.
''Ni kweli nimechaguliwa kuwa kocha wa Villa Squard hadi mwishoni mwa raundi yapili ya ligi daraja la kwanza, malengo yangu makubwa mara tu baada ya kupewa nafasi hii ni kuhakikisha timu hii kongwe inapanda ligi kuu mwakani''.
Hii leo Mwaisabula ameiongoza Villa kuifunga Ashanti mabao 2-1 kwenye mchezo wa kirafiki uliopigwa kwenye uwanja wa karume jijini Dar Es Salaam.
Je wajua ?
Hatimae CHELSEA WAKUBALI OFA YA £37M KUTOKA MAN UNITED KWA AJILI YA MATA - KUFANYIWA VIPIMO LEO

Ofa ya Manchester United ambayo inaaminika kuwa kiasi cha £37m, imekubaliwa na klabu ya Chelsea kwa ajili ya usajili kiungo wa kihispania Juan Mata.
Kiungo mwenye miaka 25 atafanyiwa vipimo vya afya leo Alhamisi kabla ya kukamilisha usajili wake wa kujiunga na mabingwa hao wa EPL.
Monday, 20 January 2014
MALINZI AELEZEA MIKAKATI YAKE KWA LOWASSA
Rais wa Shirikisho la Mpira wa Miguu Tanzania (TFF), Jamal Malinzi amesema shirikisho lake limepanga malengo ya muda mfupi na mrefu ikiwa na sehemu ya mkakati wa kuendeleza na kuinua kiwango cha mchezo huo nchini.
RAIS KIKWETE AMUAPISHA JUMA NKAMIA NA WENZAKE KUANZA KAZI RASMI

Rais Jakaya Kikwete, akimuapisha Juma Nkamia, kuwa Naibu Waziri wa Habari, Vijana Utamaduni na Michezo, katika hafla fupi iliyofanyika kwenye Viwanja vya Ikulu, jijini Dar es Salaam, leo. Picha na OMR
MANCHESTER CITY KUKIPIGA NA WEST HAM LEO.
Timu ya Manchester City leo itapambana na timu ya West Ham United katika uwanja wa Upton Parkkwenye mzunguko wa pili wa nusu fainali ya kombe la '' Capital One Cup''.
Sunday, 19 January 2014
ETO'O AUA SHETANI DARAJANI...MAN UNITED YALALA 3-1 KWA CHELSEA
MCAMEROON Samuel Eto'o amelichangamsha Jiji la London leo baada ya kufunga mabao yote matatu katika ushindi wa 3-1 wa Chelsea dhidi ya Manchester United, Uwanja wa Stamford Bridge.
Eto'o alifunga mabao mawili kipindi cha kwanza dakika ya 17 na 45 na baadaye dakika ya nne tangu kuanza kipindi cha pili akakamilisha hattrick yake kabla ya kumpisha Fernando Torres dakika ya 79.
Javier Hernandez 'Chicharito' aliyetokea benchi dakika ya 56 kuchukua nafasi ya Ashley Young aliwafungia Mashetani Wekundu bao la kufutia machozi dakika ya 78.
Nemanja Vidic alionyeshwa kadi nyekundu dakika ya 90 na ushei na Man United ikaishiwa nguvu kabisa.
Ushindi huo, unaifanya The Blues ya Jose Mourinho ifikishe pointi 49 baada ya kucheza mechi 22, ikiwa katika nafasi ya tatu nyuma ya Manchester City pointi 50 na Arsenal pointi 51, wakati United ya David Moyes inabaki nafasi ya saba pointi 37.
Katika mchezo uliotangulia, Tittenham Hotspur imeifunga Swansea City mabao 3-1 nyumbani kwake. Mabao ya Spurs yalifungwa na Emmanuel Adebayor dakika ya 35 na 71 na Chico aliyejifunga dakika 53, wakati la wenyeji la kufutia machozi lilifungwa na Bony dakika ya 78.

Shujaa: Samuel Eto'o akishangilia raha aliyowaha Chelsea na huzuni aliyowaachia Manchester United Uwanja wa Stamford Bridge leo

MANJI AWAOMBA WADHAMINI WA KLABU HIYO KUANGALIA UPYA MKATABA WA AZAM TV,ASISITIZA KUTOTETEA NAFASI YAKE
Mwenyekiti wa Yanga Yusuf Manji amewaomba wadhamini wa klabu hiyo, kuangalia upya mkataba wa Azam TV, kwani kwake yeye binafsi anauona hauna manufaa kwa klabu yao ambayo inaingiza zaidi ya mil 300 katika mchezo mmoja akitolea mfano mchezo kati yao na Watani zao Simba.
BREAKING NEWS; BARAZA JIPYA LA MAWAZIRI HILI HAPA,ASHA MIGIRO,NKAMIA NA SAADA WAULA,NCHIMBI,KAGASHEKI OUT, MAGUFULI APETA.
Dakika chache zilizo pita katibu kiongozi wa Serikali ya Tanzania kwa niaba ya raisi Kikwete ametangaa baraza jipya la mawaziri.HAYA NI MABADILIKO MAPYA
Wizara ya katiba na sheria ni Dk. Asha Migiro huku aliekuwa naibu akiendelea.
Wizara ya makamo wa raisi nchi na Mungano mabadiliko ni kwa naibu amabae ni ALL MWALIMU
Subscribe to:
Posts (Atom)