Pages

ELIMU KWANZA.

ELIMU KWANZA.
FEDHA SIO KIPAUMBELE CHETU.

Sunday, 29 December 2013

MAGOLIKIPA WA LIGI KUU YA VODACOM WAIFUNGA CLOUDS MEDIA MABAO 3-1.


Wachezaji wa timu ya Clouds Media Group wakifanya mazoezi mepesi kabla ya kuanza kwa mtanange wa kufunga mwaka dhidi ya timu ya magorikipa wanaocheza Ligi Kuu ya soka tanzania Bara.

Mbwiga akijifua.

Kocha mchezaji wa timu ya Clouds Media Group, Mbwiga Mbwiguke (kulia) akiwaongoza wachezaji wenzake katika mazoezi.

Friday, 27 December 2013

TAZAMA MAYWEATHER 'ALIVYOWATANDIKA' PACQUIAO, AMIR KHAN NA MAIADANA

BONDIA Floyd Mayweather amefufua vita ya maneno na mpinzani wake, Manny Pacquiao pamoja na kuwakandia pia Amir Khan na Marcos Maidana kwa staili ile ile. Pamoja na kumuita Pacquiao majeruhi wa Juan (Manuel) Marquez akikumbushia kipigo cha Mfilipino huyo mwishoni mwa mwaka 2012 kwa Knockout (KO) kutoka kwa Mmexico huyo, Mayweather ameweka picha ya 'kubumba' akiwa amemsukumia konde zito usoni. "Sasa unaniambia nakwenda kula makombo ya Juan Marquez? Acha nizungumze na IRS juu ya hili," alitweet mbabe huyo.

NEYMAR NOUMAAAA, APIGA TANO PEKE YAKE MECHI LA HISANI LA MASTAA BRAZIL

WAKATI La Liga ikiwa mapumzikoni, nyota wa Barcelona, Neymar alitumia nafasi hiyo kurejea Brazil kushiriki mchezo maalum wa hisani dhidi ya mchezaji wa zamani wa Paris Saint-Germain na AC Milan, Leonardo.

Marafiki wa Neymar waliwafunga Marafiki wa Leonardo mabao8-6 huku Neymar akifunga mabao matano na kuonyesha uwezo mkubwa sana wa kandanda pamoja na kuonyesha tattoo yake mpya.
Mchezaji huyo mwenye umri wa miaka 21 atarejea Hispania mapema Januari akidhamiria kuiongoza Barca katika mashindano ya nyumbani na Ulaya kwa mafanikio, kabla ya kwenda kwenye Fainali za Kombe la Dunia nyumbani kwao, Julai mwakani.


Kitu kipya: Neymar ameonyesha tattoo yake mpya wakati wa mechi ya hisani mjini Goiania, Brazil

BAADA YA KATIBU MKUU - MSEMAJI WA SIMBA NAE AACHIA NGAZI MSIMBAZI



Thursday, 26 December 2013

WENGI WAJITOKEZA KUUGAGA MWILI WA ALIYEKUWA KOCHA WA MAKIPA SIMBA MAREHEMU JAMES KISAKA yupo pia Jacob Steven JB

Jeneza lenye mwili wa aliyekuwa Kocha wa makipa wa Simba, marehemu James Kisaka likiingizwa kwenye basi la klabu hiyo, baada ya kutolewa heshima za mwisho katika misa iliyofanyika katika Kanisa la Muhimbili, Dar es Salaam. Marehemu Kisaka atasafirishwa kwenda kwao wilayani Muheza, Tanga kwa mazishi yatakayofanyika kesho. PICHA ZOTE NA KAMANDA WA MATUKIO BLOG

LUNYAMILA AENDELEA KUPATA NAFUU....

Viongozi wa Young Africans Sports Club pamoja na wachezaji wa zamani walipomtembelea kumjulia hali mchezaji Edibily Lunyamila katika hospitali Mwananyamala Disemba 24 mwaka huu.
Lunyamila anasumbuliwa na tatizo la mapafu, hali yake kwa sasa inaendelea vizuri.
Young Africans Sports Club tunamuombea Lunyamila apate nafuu ya haraka na kupona kabisa aweze kuendelea na shughuli zake za kila siku.

Abdallah Bin Kleb, Mohamed Bhinda, Juma Kaseja, Dr Nassoro Ally Matuzya, Kaise Edwin wakiwa nje ya wodi aliyolazwa mchezaji Edibily Lunyamila siku moja kabla ya Xmass wallipokwenda kumjulia hali

MISS TANZANIA 2013 ASHEREHEKEA SIKUKUU YA X - MASS PAMOJA NA WATOTO YATIMA MOROGORO


Miss Tanzania 2013 Happiness Watimanywa Akikabidhi zawadi waliotoa katika kituo hicho kwa Mama Mkuu wa Wa shirika la Masista wa Moyo safi wa Maria Sista Flora Chuma..

JAMES KISAKA AFARIKI DUNIA,


Shirikisho la Mpira wa Miguu Tanzania (TFF) limepokea kwa masikitiko kifo cha aliyekuwa kocha wa makipa wa Simba, James Kisaka (57) kilichotokea leo asubuhi (Desemba 25 mwaka huu) katika Hospitali ya Burhani, Dar es Salaam.
Msiba huo ni mkubwa katika familia ya mpira wa miguu kwani Kisaka kabla ya kuwa kocha alikuwa mchezaji katika nafasi ya kipa. Mbali ya Simba, timu nyingine alizowahi kudakia ni Ndovu ya Arusha, Volcano ya Kenya na Small Simba ya Zanzibar.

Logarusic: Mkinipa Yanga nafukuza mabeki wote



Kocha Mkuu wa Simba,Zdravko Logarusic.PICHA|MAKTABA
KOCHA Mkuu wa Simba, Zdravko Logarusic, amempa pole mwenzake wa Yanga, Ernest Brandts, kwa kupewa notisi na uongozi wa timu hiyo, lakini akasema angekuwa anaifundisha Yanga angewatimua mabeki wanne wa kikosi hicho wakiwamo nahodha Nadir Haroub ‘Cannavaro’ na Kelvin Yondani.

Katibu mpya TFF aingia na mikwara



Katibu Mkuu mpya wa Shirikisho la Soka Tanzania (TFF), Selestine Mwesigwa.
By Elius kambili,Mwananchi
KATIBU Mkuu mpya wa Shirikisho la Soka Tanzania (TFF), Selestine Mwesigwa, ameliambia Mwanaspoti kuwa jambo atakaloanza nalo akiingia ofisini ni kuziba mirija yote ya watu kujipatia fedha isivyo halali kupitia shirikisho hilo.