Pages

ELIMU KWANZA.

ELIMU KWANZA.
FEDHA SIO KIPAUMBELE CHETU.

Tuesday, 24 December 2013

MOHAMED MATUMLA NASIBU RAMADHANI KUMARIZA UBISHA CHRXMAS


Bondia Mohamed Matumla kushoto na Nassibu Ramadhani wakitunishiana misuli baada ya kupima uzito kwa ajili ya mpambano wao leo katika

ukumbi wa friends corner hotel manzese Dar es salaam leo katikati ni promota wa mpambano huo kaike siraju Picha na www.superdboxingcoach.blogspot.com



Promota kaike Siraju akiwainua juu mikono Bondia Mohamed Matumla kushoto na Nassibu Ramadhani kwa ajili ya mpambano wao wa kugombea pikipiki siku ya sikukuu ya Xmasi Picha nawww.superdboxingcoach.blogspot.com

Simba wajazwa ‘manoti’

Dar es Salaam. Uongozi wa Simba umewazawadia wachezaji wake kitita cha Sh60 milioni baada ya kufanikiwa kuichapa Yanga mabao 3-1 katika pambano la Hisani lililopigwa kwenye Uwanja wa Taifa, Dar es Salaam mwishoni mwa wiki.

Akizungumza jijini jana, Mjumbe wa Kamati ya Utendaji ya Simba, Sued Nkwabi alisema, fedha hizo zimetolea kama njia moja wapo ya kuonyesha kuthamini juhudi zilizofanywa na wachezaji hao na kufanikiwa ushindi.Simba Sports Club

MECHI YA MTANI JEMBE YAINGIZA MIL 422/-



Mechi ya Nani Mtani Jembe kati ya Yanga na Simba iliyochezwa juzi (Desemba 21 mwaka huu) Uwanja wa Taifa, Dar es Salaam na Simba kuibuka na ushindi wa mabao 3-1 imeingiza sh. 422,611,000.

Mapato hayo ni kutokana na washabiki 52,589 waliokata tiketi kushuhudia mechi hiyo kwa viingilio vya sh. 5,000, sh. 7,000, sh. 10,000, sh. 15,000, sh. 20,000 na sh. 40,000. Kiingilio cha sh. 5,000 ndicho kilichovutia watazamaji wengi ambapo walikuwa 19,044.

Monday, 23 December 2013

HII NDIO TAARIFA RASMI YA KUFUKUZWA KOCHA WA YANGA ERNST BRANDTS



Uongozi wa klabu ya Young Africans SC
umempatia taarifa (Notice) ya siku ya
thelathini (30) kocha mkuu mholanzi Ernie
Brandts juu ya kusitisha mkataba wake
kuanzia jana Disemba 22 mwaka huu.
Maamuzi hayo yanafuatia muenendo wa
matokeo mabaya katika michezo iliyopita
ya Ligi Kuu, kirafiki na bonanza la Nani
Mtani Jembe dhidi ya Simba SC mwishoni
mwa wiki.

England,RATIBA: MICHEZO YA LIGI KUU SIKU YA BOXING DAY NA MWISHO WA MWAKA HUU


 DECEMBER 29 2013

IN CENTRAL AFRICA TIME(CAT)

Thursday 26 December 2013

Hull City v Manchester United The KC Stadium 14:45

Aston Villa v Crystal Palace Villa Park 17:00

Cardiff City v Southampton Cardiff City Stadium 17:00

BREAKING NEWZ: LUNYAMILA MAHUTUTI MWAANYAMALA


WINGA wa zamani wa Yanga na Taifa Stars, Edibily Lunyamila leo hii asubuhi amekimbizwa katika hospitali ya Mwananyamala baada ya kusumbuliwa na kifua na sasa anapumua kwa msaada wa mashine.

Mtandao huu ulifanikiwa kufika hospitalini hapo muda mfupi baada ya winga huyo kukimbizwa hospitalini hapo baada ya kuzidiwa tangu jana usiku akiwa nyumbani kwake Mbezi jijini Dar es Salaam.

SOMA HABARI KAMILI http://hakileo.blogspot.com/2013/12/breaking-newz-lunyamila-mchezaji-wa.html#more

Mgimwa azushiwa kifo, Kikwete apasua kichwa

Na tanzania daima.
WAKATI mawaziri wanne wameng’olewa na wengine walioitwa mizigo wanatarajiwa kutimuliwa wakati wowote, Rais Jakaya Kikwete yupo katika wakati mgumu wa kusaka warithi wa nafasi hizo, Tanzania Daima limebaini.

Ugumu wa kusaka warithi wa mawaziri hao, umeongezeka zaidi jana baada ya Waziri wa Fedha na Uchumi, Dk. William Mgimwa kuzushiwa kifo kutokana na afya yake kuzorota.

SOMA HABARI KAMILI
  http://hakileo.blogspot.com/2013/12/mgimwa-azushiwa-kifo-kikwete-apasua.html#more

MANJI AWAOMBA WANACHAMA WA YANGA WASIVUNJIKE MOYO



Mwenyekiti wa Yanga Bw.Yusuf Manji akiongea na waandishi wa habari makao makuu ya klabu, kushoto ni makamu mwenyekiti Clement Sanga

Mwenyekiti wa klabu ya Young Africans Bw. Yusuf Manji amewaomba wanachama, wapenzi na washabiki wasivunjike moyo kwa matokeo ya jana ya mchezo wa kirafiki dhidi ya ya Simba SC, mechi iliyochezwa katika dimba la Uwanja wa Taifa jijini Dar es salaam.

Hatima ya Rage kujulikana leo

NA MWANANCHI
Dar es Salaam. Hatma ya Mwenyekiti wa Simba, Ismail Aden Rage itajulikana leo wakati kamati ya utendaji ya Shirikisho la Soka Tanzania (TFF) chini ya mwenyekiti wake Jamal Malinzi atakapokutana Uwanja wa Taifa, Dar es Salaam.
Kikao hicho mbali na kumjadili Rage pia kitapitia ajenda mbalimbali ikiwemo uundwaji wa vyombo vya haki Kamati ya Nidhamu, Kamati ya Maadili na Kamati ya Uchaguzi.

LIVERPOOL KAMA SIMBA SC, YAUA 3-1 SUAREZ APIGA MBILI



Mshambuliaji wa Liverpool, Luis Suarez akishangilia baada ya kufunga bao la pili dhidi ya Cardiff Uwanja wa Anfield leo

MSHAMBULIAJI Luis Suarez ameendeleza makali yake baada ya kufunga mabao mawili katika ushindi wa Liverpool wa 3-1 dhidi ya Cardiff jioni hii Uwanja wa Anfield.

Sunday, 22 December 2013

Bayern klabu bingwa ya dunia



Bayern Munich wamejiongezea taji jingine baada ya kuwafunga Raja Casablanca ya Morocco 2-0 na kutwaa Kombe la Klabu Bingwa ya Dunia.
Katika mechi iliyopigwa jijini Marrakech kwenye falme ya Morocco, Wajerumani hao walijawa furaha kuongeza kombe hilo katika hazina yao
ambayo tayari ina makombe ya ubingwa wa Ulaya,