Sunday, 20 October 2013
YANGA JUU TAIFA HIVI SASA
YANGA MOJA SIMBA BILAAA
GOLI LA YANGA LIMEFUNGWA NA MRISHOB NGASA.
KIPINDI CHA KWANZA AMBACHO HADI SASA HAKIJAMALIZIKA
GOLI LA YANGA LIMEFUNGWA NA MRISHOB NGASA.
KIPINDI CHA KWANZA AMBACHO HADI SASA HAKIJAMALIZIKA
Picha 5 za yule shabiki Steven wa Yanga alielia, akijiandaa kwenda kwenye mechi leo Picha 5 za yule shabiki Steven wa Yanga alielia, akijiandaa kwenda kwenye mechi leo
Ni muda umepita toka hiyo mechi ambapo leo tena Yanga na Simba kwenye uwanja wa taifa zinakutana ambapo Steven alipita mbele ya Camera ya millardayo.com na kuzungumza machache kuhusu hii mechi ya leo.
ADNAN JANUZAJ: MJUWE HUYU; ANAMILIKIWA NA MAN UNITED, ANAFUKUZIWA NA ENGLAND...MTOTO WA WAKIMBIZI WA VITA KOSOVO ALIYEZALIWA BELGIUM

Mjadala unaohusu ni nchi gani ambayo Adnan Januzaj anapaswa kuchagua kuichezea umeshika hatamu nchini England kuliko sehemu nyingine yoyote.
Wiki iliyopita kituo cha TV cha Albania kilikuwa na mjadala kuhusu nyota huyo wa Manchester United katika kipindi walichokipa jina la Hero or Traitor (Shujaa au Msaliti), kwa mtazamo atakuwa shujaa akiichagua nchi hiyo au msaliti atakapoikacha na kuchagua sehemu nyingine.
NIMEIJUA NA KUWA MPENZI WA SIMBA TANGU NIKIWA NA MIAKA SITA. NA NIMEWAFAHAMU YANGA TANGU WAKATI HUO.
Na msimu huu nimewaona Yanga na Simba wakicheza, tena na timu dhaifu kabisa, lakini, niweke wazi, kuwa kiwango cha soka kilichokuwa kikionyeshwa na Yanga ' B' na Simba ' B' enzi hizo ni cha juu zaidi kuliko Yanga na Simba ya leo.
Ni pale unapoangalia mechi ya Simba au Yanga halafu unaamua uchukue gazeti lililo mezani usome. Kwamba mchezo wa Simba au Yanga haumfanyi mtazamaji asahau kufanya mengine. Wanacheza soka iliyopooza.
Friday, 18 October 2013
Picha 10 kutoka kwenye video mpya ya “Kimugina” ya Linex aliyoonekana na huyu mrembo Jackline Patrick
Ameongea na millardayo.com na kusema “Kesho kwenye uzinduzi wa video ya Kimugina kutakuwa na red carpet pamoja na show nzima kusimamiwa na Irene Uwoya na Kajala, Wema Sepetu na mastaa wengine wa bongomovie watafika siku hiyo pia watakaonisindikiza ni Barnaba boy, Chid Benz na wengine’
Huyu ndio msanii wa pili aliethibitishwa kushuka kwenye Fiesta 2013
TANZANIA YAPOROMOKA VIWANGO FIFA
Shirikisho la Soka la Dunia (Fifa) limetangaza viwango vipya vya ubora wa soka kwa Oktoba, huku Tanzania ikiporomoka kwa nafasi mbili kutoka ile ya 128 hadi 130.
Licha ya kuporomoka, pia Tanzania imejikuta ikikamata mkia kwa ubora wa soka miongoni mwa nchi tano za Jumuiya ya Afrika Mashariki.
YANGA yaota "TUTAIPIGA SIMBA 3-0 J`PILI"
Mabingwa wa Tanzania Bara, Yanga wamesema wamejipanga kuhakikisha wanaibuka na ushindi wa 3-0 dhidi ya watani wao wa jadi, Simba katika mchezo wa Ligi Kuu ya Vodacom Tanzania Bara utakaopigwa keshokutwa kwenye Uwanja wa Taifa jijini Dar es Salaam.
Akizungumza na waandishi wa habari baada ya kumalizika kwa kikao cha Kamati ya Utendaji, Baraza la Wazee na matawi ya Yanga ya jiji la Dar es Salaam kilichofanyika kwenye ofisi za makao makuu ya klabu hiyo jijini jana, msemaji wa matawi hayo, Bakili Makele alisema mipango ya 'kumuua mnyama' imeshakamilika na wameshahakikishiwa kuibuka na ushindi wa magoli 3-0 katika mchezo huo mgumu dhidi ya vinara wa ligi.
JANUZAJ KUBAKI MAN U, ANATAKA KUWA MCHEZAJI BORA WA DUNIA
KINDA Adnan Januzaj amesema kwamba anataka kuongeza Mkataba kuendelea kucheza Manchester United.
Kijana huyo mwenye umri wa miaka 18, alifunga mabao mawili dhidi ya Sunderland katika mchezo wake wa kwanza wa Ligi Kuu England kwa mabingwa hao watetezi na anatarajiwa kusaini Mkataba wa muda mrefu Old Trafford.
Mkataba wa sasa wa Januzaj unatarajiwa kumalizika Juni 2014 na vigogo wa Ulaya, Juventus na Barcelona wanataka saini ya kiungo huyo, lakini anatarajiwa kubaki United na kusaini Mkataba mpya.
"Nina furaha Manchester United na ninataka kujifunga kwa asilimia 100 kufanya vizuri katika kila mechi," Januzaj aliiambia Shirika Televisheni ya Kosovo, KTV.
Subscribe to:
Posts (Atom)
