Pages

ELIMU KWANZA.

ELIMU KWANZA.
FEDHA SIO KIPAUMBELE CHETU.

Friday, 18 October 2013

UFAHAMU,Mlo Bora Kwa Mama Mjamzito Sehemu Ya Kwanza

Kwa ajili ya afya ya mama na mtoto ni muhimu sana mwanamke apate chakula bora. Ukosekanaji wa chakula bora kunaweza kukasababisha mtoto kuzaliwa kabla ya mda wake au na uzito mdogo ambao unaweza ukachangia katika kuzuia ukuaji wa ubongo na mwili.

Kwa mama anaweza akapata anaemia, infection, matatizo katika placenta, matatizo katika labor, c-section(kuzaa kwa upasuaji wakati wa kujifungua), kutokupona kwa haraka, matatizo katika kunyonyesha, toxemia na pre-eclempisa(haya ni magonjwa yanayosababishwa na maini kutoweza kufanya kazi yake vizuri na mwili kujitahidi kutoa protein kutoka sehemu nyingine za mwili kwa sababu hamna protein ya kutosha).


Dalili zake ni pamoja na kuwa na protein kwenye mkojo, blood pressure kuwa juu, kuumwa kwa kichwa, kusikia kizungu zungu, kuzimia, kuvimba kwa viungo n.k





Mama mjamzito anatakiwa apate 100 grams za protein kwa siku.
Ifuatayo ni mlo kamili anaotakiwa apate mama mjamzito kila siku ya ujauzito wake kwa afya bora:


Maziwa na vyakula vya jamii ya maziwa: Glasi nne au zaidi ya maziwa ya aina yoyote pamoja na/au vyakula vyenye jamii ya maziwa kama jibini, mtindi,siagi, ice cream. Maziwa ni muhimu kwa protein, calcium, vitamins na virutubisho vingi. Vitasaidia ukuaji wa mifupa, misuli na nerves. Ni muhimu kwa damu yenye afya, kusaidia usingizi na kusawazisha mdundo wa moyo.

MAMBO YAMEWIVA,MISS UNIVERSE TANZANIA AKABIDHIWA BENDERA LEO





Mrembo wa Miss Universe Tanzania 2013 Betty Boniface Omara amekabidhiwa bendera leo na waziri wa mali asili na utalii mheshimiwa Kagasheki.

Zoezi hili limefanyika katika ukumbi wa mkutano wa wizara hiyo tayari kwa safari yake ya kwenda kwenye mashindano ya Miss Universe yatakayofanyika Moscow nchini Urusi mapema mwezi Novemba.

BREAKING NEWS; KAMATI YA UCHAGUZI TFFF YA MUENGUA TENA SHAFFIH DAUDA.


KAMATI YA TFF IMEENGUA TENA JINA LA MTANGAZAJI WA MICHEZO WA SPORT EXTRA YA CLOUS FM.

KWA MARA YA KWANZA KISINGIZIO ILIKUWA NI UZOEFU ILA SASA  ILA SABABU KUBWA HAIJA JULIKANA , BAADAE ALIPEWA ADHABU KWA UTOVU WA MAADILI NA HATIMAE KUPELEKWA KWENYE KAMATI YA MAADILI AMBAKO ALIPEWA ADHABU YA KULIPA MILIONI MOJA FEDHA ZA KITANZANIA.

 ILA KWA SASA KAMATI HUSIKA IMELIENGUA RASIMI JINA LAKE KATIKA UCHAGUZI MKUU UNAOTARRAJIWA KUFANYYIKA SIKU KADHAA ZIJAZO.
kwa muendelez wa Habari hii endelea kutufwatilia....
www.tabasamuleo.blogspot.com



JE, WAJUA BAADA YA MESSI, RONALDO NA NEYMAR ANAYEFUATIA KWA UBORA DUNIANI NI BALOTELLI




GWIJI wa soka duniani, Diego Maradona

Mario Balotelli

GWIJI wa soka duniani, Diego Maradona amesema kwamba Mario Balotelli ni mwanasoka nambari nne kwa ubora hivi sasa duniani baada ya Messi, Ronaldo na Neymar.Katika kipindi cha maswali na majibu mjini Milan, gwiji huyo wa Argentina alielezea mapenzi yake kwa nyota huo wa zamani wa Manchester City na kwamba walianza kufahamiana vyema na mshambuliaji huyo wa Italia alipomtumia picha anavuta cigar ya Cuba.

Namba 10 huyo wa zamani, mmoja wa wanasoka bora kabisa kuwahi kutokea duniani alisema: "Mawasiliano yangu ya kwanza na Mario ni pale aliponitumia picha yake anavuta Cuban. Naipenda! Nilicheza,".

MAKALA: ONAJINSI HADITHI YA UWANJA SIMBA ILIVYOHAMIA YANGA



Na Elius Kambili

MWENYEKITI wa klabu ya Simba, Ismail Aden Rage aliposema hivi karibuni kuwa "Kama serikali imeweza kujenga uwanja wa kisasa (wa taifa) kwa muda wa miaka 50, iweje mimi niweze ndani ya miaka miwili?" alimaanisha uwanja alioahidi kuujenga sasa haiwezekani.

Rage alitoa ahadi hiyo alipoingia madarakani Mei, 2010. Aliahidi kuendeleza mchakato wa ujenzi wa uwanja huo, eneo Bunju, Dar es Salaam.

Lakini kwa kauli hiyo mpya ilimaanisha Simba haiwezi kujenga uwanja wake kwa sasa. Macho na masikio ya wadau wa soka yalielekezwa kwa watani wao Yanga, klabu iliyofikia hatua hata ya kuonyesha michoro ya uwanja na kuunda kamati maalum kwa ajili ya ujenzi huo.

Yanga walikuja na wazo hilo mwaka 2010 kwamba itajenga uwanja wa kisasa katika eneo la Jangwani yalipo makao makuu ya timu hiyo makutano ya mitaa ya Jangwani na Twiga.

MBARAKA MWINSHEHE NDIYE ‘FRANCO WA AFRIKA MASHARIKI’



KWA MUJIBU WA BLOGU YA BOTHER DANNY

Machi 17, 1973 Mbaraka akimvisha pete mkewe Amne. Picha kwa hisani ya Kijiwe cha Kitime.
Kupanda kwa bei ya mafuta kulimkimbiza Moro Jazz 1973
Na Daniel Mbega

MOROGORO kuna vipaji vingi – kuanzia soka, ndondi na muziki. Huko ndiko walikotokea akina Leodgar Tenga, Hashim Kambi, golikipa wa zamani wa Sunderland Mbaraka Salum Magembe, Hassan Mlapakolo, Adam Sabu na wengineo ni baadhi tu ya wanasoka waliotoka Morogoro.
Hivi karibuni tu bondia kutoka Morogoro, Francis ‘Maputo’ Cheka alitwaa ubingwa wa dunia kuonyesha kwamba vipaji vya ndondi vimekuwepo kwa miaka mingi tangu enzi zile za klabu za shule za sekondari za Forest Hill na Mzumbe.
Lakini ukizungumzia muziki, hapo nadhani ndipo mahala pake. Walikuwepo akina Salim Abdallah Yazidu ‘Say’ aliyetamba na bendi za Cuban Marimba na Moro Jazz pamoja na ‘Mfalme’ wa gitaa za solo nchini Tanzania, Mbaraka Mwinshehe Mwaruka. Lakini pia tumeshuhudia wanamuziki wengi wa Bongo Fleva wakiinukia huko kama ‘Mfalme wa Rhymes 2004’ Selemani Msindi ‘Afande Sele’ na akina Mdogo Ditto na Belle 9.

Thursday, 17 October 2013

ONAJINSI YANGA ILIPOCHAPWA 4 MBELE YA KAWAWA




Mzee Hamisi Ally Kilomoni, mchezaji wa zamani wa Sunderland anayekumbukwa na Yanga kwa jinsi alivyokuwa anapachika mabao dhidi yao. Picha kwa hisani ya Bin Zubeiry.

SUNDERLAND, ambayo wakati huo ilikuwa ikishikilia ubingwa wa kandanda wa Afrika Mashariki ‘Allsopps Cup’ pamoja na ubingwa wa Taifa, Jumapili ya Mei Mosi, 1966 iliinyoa Yanga bila maji kwa kuifunga magoli 4-0 katika Uwanja wa Ilala, mbele ya waheshimiwa Makamu wa Pili wa Rais, Rashid Mfaume Kawawa, Mawaziri, Mabalozi, Mkuu wa Mkoa wa Pwani, Selemani Kitundu na

MABAO 156, MECHI 75 ZA SIMBA NA YANGA LIGI KUU

Furaha ya ubingwa kwa Simba 2012 huku wakisherehekea ushindi wa mabao 5-0 dhidi ya mahasimu wao, Yanga.
Na Daniel Mbega
HUKU utasikia: “Simba! Simba! Simba!” halafu kule nako kutasikika: “CCM! CCM! CCM!” Naam, hivi ni vibwagizo vinavyosikika kila wakati Simba na Yanga zinapokutana, iwe kwenye mechi za Ligi, mashindano mbalimbali na hata zile za kirafiki.
Mashabiki wa Simba wanaweza kusikika pia wakisema: “Amesimama kidedea, eeee kidedea!” halafu upande mwingine utawasikia wakichombea: “Kitimtimu, mtakiona leo, nyumba ya shetani mwendawazimu kaingiaje!”

JOHARI, UWOYA ‘WATELEKEZWA’ BAA

Stori: Jelard Lucas
NYOTA wa sinema za Kibongo, Blandina Chagula na Irene Uwoya wamedaiwa kutelekezwa katika Baa ya Miles Stone, Arusha.
Kwa mujibu wa chanzo chetu, wawili hao walifika katika baa hiyo hivi karibuni na kuwasubiri vibosile maarufu wa madini ili waweze kula bata lakini wakawatelekeza hivyo wakabaki peke yao bila kuwa na vinywaji mezani.
Johari alipoulizwa kuhusiana na tukio hilo, alisema: “Hayo ni mambo ya blogu, mbona nina muda sana tangu nitoke Arusha, ipotezee hiyo habari.”

MAMBO MUHIMU AMBAYO MWANAMKE HUITAJI KUTOKA KWA MUWEME



NI matumaini yangu kuwa umzima na unaendelea vyema na majukumu yako ya kila siku kama kawaida. Wiki iliyopita utakumbuka niliishia kuzungumzia suala la busara. Nikasema mwanamke anaweza kuwa chanzo cha furaha kwa mumewe endapo atatumia busara kwa kiwango kinachotakiwa.

Kwa kifupi wanaume wanahitaji sana busara ya mwanamke na kama mwanamke ukiweza kuwa na busara katika kumtatulia matatizo yake hata kwa kumpa mawazo yako na kumpa moyo, ataona umuhimu wako na wakati mwingine kukushirikisha kila afanyalo kabla ya kulifanya hasa baada ya kuona anaishi na mwanamke mwenye busara.

KUMEKUCHA, Makocha wagwaya kutabirli Simba, Yanga

Dar es Salaam. Makocha wa timu za Ligi Kuu Tanzania Bara wamepatwa na kigugumizi kutabirlia matokeo ya mechi ya watani wa Simba na Yanga itakayopigwa Jumapili ijayo kwenye Uwanja wa Taifa, Dar es Salaam.
Wakizungumza na Mwananchi katika mahojiano maalumu kocha Mkuu wa Mbeya City, Juma Mwambusi alisema amebahatika kuziona na kuzielezea kiufundi.

“Kwa bahati nzuri Simba na Yanga tayari tumecheza nao nimewaona ni wazuri wapi na udhaifu wao uko wapi. Kiufundi hazitofautiania sana. Simba ina wachezaji wa kigeni wanne kwenye kikosi chake cha kwanza sawa na Yanga, nafikiri viwango vyao vinalingana, hakuna tofauti kubwa.”

Nyota wa kigeni wa Yanga ni Mbuyu Twite, Haruna Niyonzima, Hamis Kiiza na Didier Kavumbagu wakati Simba ina Abel Dhaira, Joseph Owino, Gilbert Kaze na Amis Tambwe.