Mshambuliaji Wayne Rooney amesisitiza ameshukuru kuona England imefanikiwa kufuzu kwa Kombe la Dunia mwakani Brazil.
Rooney sasa amepata nafasi nyingine ya kuonyesha kipaji chake katika mashindano makubwa baada ya kufunga bao la kwanza na kuiongoza England kushinda 2-0 dhidi ya Poland kwenye uwanja wa Wembley.
Rooney anajua England ina nafasi ya kufanya makubwa Brazil kama akiendelea kucheza kwa kiwango cha juu hadi wakati huo.

