Pages

ELIMU KWANZA.

ELIMU KWANZA.
FEDHA SIO KIPAUMBELE CHETU.

Thursday, 3 October 2013

PATA MATOKEO YA LIGI YA MABINGWA WA ULAYA:





CSKA Moskva 3 - 2 Viktoria Plzeň

Shakhtar Donetsk 1 - 1 Manchester United

Bayer Leverkusen 2 - 1 Real Sociedad

Juventus 2 - 2 Galatasaray

Real Madrid 4 - 0 København

PSG 3 - 0 Benfica

Anderlecht 0 - 3 Olympiakos Piraeus

Manchester City 1 - 3 Bayern München www.tabasamuleo.blogspot.com

Wednesday, 2 October 2013

Ferguson akanusha madai ya kwamba anataka kurejea kuifunza Timu hiyo


Kocha wa zamani wa Manchester United Sir Alex Ferguson akiwasalimia mashabiki

Kocha wa zamani wa Klabu ya Manchester United Sir Alex Ferguson amekanusa taarifa zilizokuwa zimezagaa ya kwamba yupo mbioni kurejea tena kwenye kazi yake ya kuongoza Timu hiyo kutokana na kushuhudia matokeo mabaya kwa klabu yake ya zamani. Ferguson amesema hana mpango wala nia ya kurejea tena kuwa Kocha kwani anaamini kazi yake ameshaifanya ipasavyo na sasa ataendelea kufamnya shughuli nyingine nje ya kuwa mkufunzi.

Kocha huyo mkongwe mwenye umri wa miaka 71 amesema hawezi akarejea tena nyuma eti kwa sababu Manchester United inashika nafasi ya kumi na mbili kwenye msimamo wa ligi kwani anaamini ipo kwenye mikono salama.

David Moyes atetea uamuzi wake wa kubadili wachezaji kwenye kikosi cha kwanza cha Manchester United


Kocha Mkuu wa Manchester United David Moyes akifanya mkutano wa waandishi wa habari

Kocha Mkuu wa Klabu ya Manchester United David Moyes amejitetea na kusema kwa sasa anaendelea kusaka Kikosi cha kwanza kauli aliyoitoa baada ya kukosolewa vikali na Kocha wa Shakhtar Donetsk Mircea Lucescu aliyesema hakuna sababu ya kubadili wachezaji kila siku. Moyes ambaye amekuwa akipata matokeo mabovu kwenye michezo ya Ligi Kuu nchini Uingereza amejikuta akikosolewa vikali kutokana na tabia yake ya kubadili wachezaji wa kikosi cha kwanza kitu ambacho kinatajwa kuwa chanzo cha matokeo mabaya.

Real Madrid kukosa huduma ya Mshambuliaji wake Gareth Bale kwenye mchezo dhidi ya FC Copenhagen kutokana na majeraha


Timu ya Madaktari wa Real Madrid wakitoa huduma ya matibabu kwa Mshambuliaji Gareth Bale

Kikosi cha Real Madrid kinatarajiwa kukosa kwa mara nyingine huduma na Mshambuliaji wake ghali zaidi duniani Gareth Bale anayekabiliwa na majeraha ya nyamaza za paja na hivyo hatakuwepo kwenye mchezo wa Ligi ya Mabingwa Barani Ulaya dhidi ya FC Copenhagen.

Kocha Mkuu wa Nigeria Stephen Keshi asisitiza kuendelea na mkakati wake wa kujenga kikosi imara


Nigerian Head Coach Stephen Keshi
Kocha Mkuu wa Timu ya Taifa ya Nigeria Stephen Keshi akiwa kibaruani
Kocha Mkuu wa Timu ya Taifa ya Nigeria Stephen Keshi ameweka wazi yupo kwenye harakati za kuendelea kuijenga Timu hiyo na hadi kufika sasa bado hajapata Kikosi ambacho anakihitaji.

UWANJA A TAIFA SII SALAMA.







Na Mwandishi Wetu
PAMOJA na tukio kubwa na la hatari la kutisha lililotokea katika nchi jirani ya Kenya, imebainika hakuna tahadhari yoyote iliyochukuliwa katika sehemu za mikusanyiko mikubwa ya watu kama vile Uwanja wa Taifa jijini Dar es Salaam.

ONA UFUSIKA WA WEMA NA AUNT EZEKILEL CHINA.


Na Mwandishi Wetu
LICHA ya mwaka jana kuita vyombo vya habari na kujisafisha baada ya kukaa nusu utupu jukwaani, mastaa wawili wa filamu za Kibongo, Wema Isaac Sepetu na Aunt Ezekiel wamefanya uchafu wakiwa Hong Kong, China.
Video ya aibu ya wawili hao ilivuja mitandaoni mwishoni mwa wiki iliyopita ikiwaonesha ‘wakidendeka’ na kufanyiana vitendo vinavyokwenda kinyume na maadili ya Kitanzania.

Tuesday, 1 October 2013

PATA MATOKEO YA CHAPION LEAGUE

FIESTA NI MAJANGA,WALA SIO SEHEMU YA BURUDANI


MAJANGA HAYA! NINGELIKUWA WAZIRI WA VIJANA, UTAMADUNI NA MICHEZO...



Basi, Siku ya kwanza tu ya kuingia ofisini ningetoa tamko la kupiga marufuku fiesta zote isipokuwa kwenye misimu ya likizo za wanafunzi. Na kwa masharti, kuwa fiesta kwa watoto chini ya miaka 18 zianze alasiri na kumalizika saa kumi na mbili jioni. Fiesta za usiku iwe ni kwa watu wazima tu.

Tuwe wakweli kwa jamii yetu na Nchi Yetu. Wanaosema ' Twenzetu tukawinde' wanapotosha umma. Ni sawa na kusema pia ' Twenzetu tukawindwe'. Wahenga walinena; mwinda huindwa. Hapo pichani imeandikwa, kuwa bia laki 2 kuwindwa. Ni majanga. Hapa kuna ' wawindaji haramu' wenye kuwaaminisha wenye kuwindwa kuwa wao ndio wawindaji www.tabasamuleo.blogspot.com

IRENE UWOYA ajiuzulu muve BONGO, asema HATA IGIZA TENA

"ww.tabasamuleo.blogspot.com NIMEAMUA KUACHA MAMBO YA MOVIE NA KUWAACHIA WENGINE"

Msanii maarufu wa bongo movie Irene Uwoya ameaacha rasmi kuigiza bongo movie na kuamua kundelea na shughuli zake nyingine kama TV SHOWS.


Kupitia website ya DSTV Irene Uwoya alifunguka na kusema “Nimeamua kuacha mambo ya movie na kuwaachia wengine, haya maamuzi nimeyafanya kama miezi sita iliyopita… Mara ya mwisho kuigiza ni zaidi ya miezi sita iliyopita pia.”
Movie alizocheza mpaka sasa zinafika 40 lakini za kwake ni nne tu na amekiri kwamba kuacha kwake kuigiza hakuta mshushia kipato chake cha siku zote ambapo kwa movie moja ya kwake mwenyewe alikua anaiuza mpaka kwa milioni 35.
source DSTV

Monday, 30 September 2013

YANGA YA CHANJA MBUGA SASA KUJENGA UWANJA WA KISAASA MAPEMA.


UJENZI WA UWANJA WA YANGA: TAARIFA KUHUSU MAENDELEO YA MRADI WA UJENZI


LEO tungependa kupitia kwenu kutoa taarifa kuhusu maendeleo ya mradi wetu wa Uwanja wa kisasa wa mpira katika Jiji la Jangwani kama itakavyojulikana

Mara ya mwisho tuliongea ama kuonana ilikuwa mwezi wa tatu wakati Ndugu zetu wa BCEG walipokabizi Concept design ama Usanifu wa awali na kuanzia sasa tutakuwa tunatoa taarifa za mara kwa mara kuhusu mradi huu. Wahenga walisema UKICHA KUSEMA HUTATENDA JAMBO lakini pia KUKAA KIMYA SANA kunajenga hisia mbaya na kutoa nafasi ya upotoshwaji wa habari.www.hakileo.blogspot.com