Pages

ELIMU KWANZA.

ELIMU KWANZA.
FEDHA SIO KIPAUMBELE CHETU.

Monday, 30 September 2013

NI MOTO ULAYA LEO;ARSENAL, CHELSEA, BARCA, DORTMUND, NAPOLI, AC MILAN…!!!




RAHA NI ARSENAL v NAPOLI, STEAU v CHELSEA, PORTO v ATLETICO, CELTIC v BARCA!

MECHI za Pili za Makundi E hadi H zipo Dimbani leo huku Chelsea wakiwa Ugenini wakisaka ushindi wao wa kwanza baada ya kutandikwa katika Mechi yao ya kwanza, Arsenal wapo Emirates na mtanange mkali sana na Napoli huku Vigogo Barcelona, bila ya Supastaa Lionel Messi, wakiwa Ugenini Uwanja wa Celtic Park ambako Msimu uliopita walinyukwa.(P.T)

RATIBA:

[Saa za Bongo]

Jumanne 1 Oktoba 2013

[Saa 1 Usiku]
www.hakileo.blogspot.com

Kocha wa Liverpool Brendan Rodgers ajivunia Suarez na Sturridge.



Washambuliaji wa Klabu ya Liverpool Daniel Sturridge na Luis Suarez wakishangilia moja kati ya magoli matatu waliyoshinda dhidi ya Sunderland
Na Nurdin Selemani Ramadhani

Kocha Mkuu wa Liverpool Brendan Rodgers ameibuka na kusifu timu yake ndiyo yenye safu hatari zaidi ya ushambuliaji na hili limekuja kutokana na ushindi alioupata kwenye mchezo dhidi ya Sunderland huku washambuliaji wake wawili wakifunga magoli yao matatu.www.tabasamuleo.blogspot.com

Barcelona kukosa huduma ya Lionel Messi


kwa kipindi cha majuma matatu baada ya kuumia nyama za paja





Mshambuliaji wa Barcelona Lionel Messi akishangilia moja ya magoli aliyofunga dhidi ya Ajax

Klabu ya Barcelona ya nchini Hispania inatarajiwa kukosa huduma ya Mshambuliaji wake wa Kimataifa wa Argentina na Mchezaji Bora wa Dunia Lionel Messi kwa kipindi cha majuma matatu kutokana na kusumbuliwa na maumivu ya nyama za paja.

Maumivu ya Messi aliyapata kwenye mchezo wa ligi dhidi ya Almeria ambapo Barcelona walifanikiwa kupata ushindi wa magoli 2-0 na hivyo kuendelea kujiwekea mazingira mazuri ya kutetea Ubingwa wao msimu huu.www.tabasamuleo.blogspot.com

WENGER AWAKOROMEA WACHEZAJI WAKE.




Kocha Mkuu wa Arsenal Arsene Wenger akizungumza na wanahabari na kutoa onyo kwa wachezaji wake kabla ya mchezo dhidi ya Napoli
Na Nurdin Selemani Ramadhani

Kocha Mkuu wa Vinara wa Ligi Kuu nchini Uingereza Arsenal, Arsene Wenger ametoa onyo kwa wachezaji wake kuwa makini kwenye mchezo wao wa siku ya jumanne wa Ligi ya Mabingwa Barani Ulaya watakapovaana na Napoli kutoka nchini Italia. Wenger amewataka wachezaji wake kuwa na tahadhari kwa ajili ya mchezo huo kutokana na kiwango cha Napoli kuwa kizuri na iwapo hawatakuwa makini basi huenda wakapoteza mchezo huo utakaopigwa nyumbani kwao huko kwenye Dimba la Emirates.www.tabasamuleo.blogspot.com

Roberto Mancini huenda akapewa kibarua cha kuinoa Galatasaray iwapo atakubaliana na Uongozi kwenye mazungumzo yanayoendelea






Kocha wa zamani wa Manchester City Roberto Mancini akiwajibika wakati akiwa na Klabu hiyo
Klabu ya Galatasaray ya nchini Uturuki ipo kwenye mazungumzo na Kocha wa zamani wa Manchester City Roberto Mancini kwa lengo la kumpa kibarua cha kukinoa kikosi chao kutokana na Klabu hiyo kumtimua Kocha wake.
Klabu ya Galatasaray imethibitisha kuanza mazungumzo na Mancini aliyetimuliwa nchini Uingereza baada ya kushindwa kutwaa taji lolote msimu uliopita wa Ligi Kuu na kuambulia kumaliza nafasi ya pili.www.tabasamuleo.blogspot.com

www.tabasamuleo.blogspot.comRais wa Klabu ya Galatasaray Unal Aysal pamoja na Mkurugenzi Mtendaji Lutfi Aribogan wamekutana na Mancini kwa mazungumzo kuangalia iwapo wataafikiana ili aweze kuanza kazi ya kuifundisha timu hiyo.

Galatasaray wamelazimika kuanza kibarua cha kusaka kocha mwingine baada ya kumtimua Fatih Terim juma lililopita ikiwa ni siku chache baada ya kupata kipigo cha mbwa mwizi kutoka kwa Real madrid kwenye michuano ya Ligi ya Mabingwa Barani Ulaya.

Mancini huenda akachukua nafasi ya Terim aliyefukuzwa baada ya kushindwa kufikia makubaliano na Uongozi wa Galatasaray juu ya kuongeza mkataba wa kuendelea kuifundisha Klabu hiyo.

Terim alikuwa ni mtu mwenye ushawishi mkubwa ndani ya Klabu ya Galatasaray na amefanikiwa kuipa mataji sita miongoni mwa makombe kumi na kenda ambayo timu hiyo imeshinda kwenye historia yake.

Kocha huyo wa Galatasaray anatimuliwa kipindi hiki timu hiyo ikiwa kwenye nafasi ya kumi kwenye msimamo ikiwa imecheza michezo mitano wakiwa pointi nane nyuma ya vinara wa msimu huu na mahasimu wao Fenerbache.

Mancini iwapo atatangazwa kuchukua nafasi ya Terim atakuwa na kibarua cha kuhakikisha Galatasaray inaendeleza ubabae wake kwenye ligi ya nyumbani sanjari na mashindano ya Kombe la Ulaya kwa ngazi za Klabu.

ONA JINSI Megan Young Miss Philippines alivyoibuka mshindi wa Miss World 2013


Miss kutoka Philippines Megan Young ndio amevishwa taji la Miss World 2013 iliyofanyika usiku wa jumamosi, Bali Nusa Dua Convention Center Indonesia.

"I promise to be the best Miss World ever," Alisema Miss Megan baada ya kuvishwa taji hilo na miss world 2012, Wenxia Yu.

MISS UTALII KUTANGAZA KUPATIKANA NYATI WA AJABU NGORONGORO


Nyati mweupe nayepatikana Ngorongoro (HM)

Miss Utalii Tanzania 2013, Hadija Said Mswaga, amesema kuwa kupatikana kwa nyati mweupe wa ajabu na pekee duniani katika hifadhi ya Ngorongoro, imekuwa ni chachu na kichocheo cha pekee kwake katika mpango mkakati wake wa kuitangaza Hifadhi ya Ngorongoro kitaifa na kimataifa, ambapo kwa kuanzia ameamua kuanza kampeni hiyo kupitia mashindano ya dunia anayokwenda kushiriki ya Miss Tourism World 2013, ambayo mwaka huu yanafanyikia nchini Equatorial Guinea Octoba 12, 2013.www.tabasamuleo.blogspot.com

MAAJABU,WATOTO WAFUNGA NDOA.

Wanandoa Mary Chinjendi (15) na Amos Sailowa (17).
Na Imelda Mtema
HAKUNA lugha inayofaa kutumika katika habari hii zaidi ya kusema hii ni kali ya mwaka! Katika hali ya kushangaza, watoto Mary Chinjendi (15) na Amos Sailowa (17), wazaliwa wa Kijiji cha Vilundilo Mbandee, Mkoa wa Dodoma, wamefunga ndoa huku wazazi wa pande zote mbili wakisherehekea harusi, Ijumaa Wikienda lina mkasa wote.www.tabasamuleo.blogspot.com

makala SIMBA SC 2-0 JKT: SIMBA SC NI WAZITO SANA, JAPO WANASHINDA



Na Baraka Mbolembole Mabadiliko yakumtoa nje kiungo Amri Kiemba na kumuingiza uwanjani chipukizi RamadhaniSingano, awali yalionekana kama yangeipa wakati mgumu zaidi timu ya Simba mchezoni. Ila kocha Abdallah ‘King’ Kibadeni aliendelea kuwaamini kundi la wachezaji wake vijana alionao kikosini na kupata pointi nyingine tatu muhimu na kujitanua katika kilele cha msimamo wa ligi kuu Tanzania Bara.

Azam TV kuonyesha mechi zote za Ligi kuu Bara Ikiwemo zile za Yanga



Mtaalamu wa mitambo ya kurusha mpira mojakwamoja wa kituo cha televisheni cha Azam TV akiwajibika uwanjani
KITUO cha Televisheni cha Azam kimeahidi kuonyesha mechi za Yanga zitakazochezwa katika Uwanja wa Taifa jijini Dar es Salaam na zile za ugenini kwa sababu mkataba unawaruhusu.
www.tabasamuleo.blogspot.com

ONAJINSI FRANSIC MIYEYUSHO ALIVYOMTWANGA SADIK MOMBA




Bondia Sadiki Momba kushoto akioneshana umwamba wa kutupiana makonde na Fransic Miyeyusho wakati wa mpambano wao usiokuwa wa ubingwa uliofanyika siku ya jumapili katika ukumbi wa Friends Coner Manzese.www.hakileo.blogspot.com